Sare ya jana dhidi ya Zanaco inawaweka katika mazingira magumu Yanga na ili kusonga mbele hatua ya makundi
Kocha msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi amesema uchovu waliokuwa nao wachezaji wao ndiyo imechangia timu yao kucheza chini ya kiwango katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa jana.
Mwambusi ameiambia Goal, mechi ilikuwa ngumu kwa upande wao kwasababu wachezaji walikuwa wamechoka kutokana na kucheza mechi nne kwa siku 10.
"Nawapongeza wachezaji wangu kutokana na jitihada kubwa walizozionyesha katika dakika 90, ukweli vijana walikuwa wamechoka kutokana na fatiki ratiba haikuwa rafiki kwetu ndio maana tukicheza chini ya kiwango na kupata sare," amesema Mwambusi.
Kocha huyo mzalendo amesema pamoja na sare hiyo lakini bado hawajakata tamaa warajipanga ili kwenda kushinda ugenini Zambia katika mchezo wa marudiano.
Mwambusi amesema atakwenda Zambia wakiwa wanawajua vizuri wapinzani wao Zanaco hivyo anaamini wanaweza kupata matokeo.
Kocha huyo amesema kingine kinachowapa matumaini ni kupata uhakika wa kuwatumia nyonga wao ambao A naamini watakuwa amepona vizuri baada ya kuwalazimisha kuwatumia kwenye mchezo wa jana lakini walishindwa kupambana hadi mwisho wa mchezo.
Sare ya jana dhidi ya Zanaco inawaweka katika mazingira magumu Yanga na ili kusonga mbele hatua ya makundi wanapaswa kupata ushindi wowote katika mchezo huo utakaopigwa uwanja Lusaka Zambia Jumamosi ijayo.