Bosi huyo wa United amesema kutoa sare na Arsenal ni sawa na kipigo tu, pia amedai kuwa Walcott na Sanchez si kitu dhidi ya Mashetani Wekundu
Jose Mourinho meneja wa Manchester United amekiri kuwa sare waliyopata dhidi ya Arsenal Jumamosi kwake ni sawa na kipigo.
United walifurahia nafasi nyingi dhidi ya Arsenal waliocheza chini ya kiwango, lakini Olivier Giroud aliyetikisa wavu kwa mpira wa kichwa alifuta goli la Juan Mata na kuwapatia Gunnerspointi moja.
Carrick ataja matatizo ya Manchester United
Mourinho alifurahia jinsi kikosi chake kilivyokaba sehemu kubwa ya mchezo, na amesisitiza kuwa hawana sababu ya kusononeshwa sana na goli la kusawazisha la Arsenal lililofungwa dakika za mwisho.
“Kazi ilikuwa nzuri, wachezaji wangu walifanya kazi nzuri. [Phil] Jones na [Marcos] Rojo hawakujiunga na timu zao za taifa, walibaki na kufanya kazi wiki mbili zilizopita. Wanafanya kazi vizuri sana. Antoni [Valencia] alivunjika mkono, lakini amecheza vizuri ajabu. Wachezaji mahiri kama [Alexis] Sanchez, [Mesut] Ozil, [Theo] Walcott – hatukuona kitu kutoka kwao kwa sababu uwezo wetu, wala si kwa sababu yao,” aliiambia tovuti rasmi ya klabu yake.
David Alaba kutua Manchester United majira ya joto
“Tulikuwa na nafasi nzuri: Kama [Wayne] Rooney angempigia pasi [Paul] Pogba angepata goli la wazi kabisa. Rojo alipiga kichwa goli likiwa wazi. Tulikuwa na nafasi za kutosha kuumaliza mchezo kwa ushindi wa 2-0 lakini tuliambulia patupu, 1-1. Wachezaji wapo kimya. Wanahisi wamefungwa na wamevunjika moyo sana.
“Lakini nimewaambia, hisia mbaya zaidi ni pale unapojichukia mwenyewe kwa sababu hukucheza katika kiwango kinachotarajiwa au ulifanya makosa makubwa, lakini hawawezi kuwa na hisia hiyo. Wanastahili kujivunia kile walichofanya, lakini katika uhalisia wamevunjika moyo sana kwa sababu tumepoteza pointi mbili dhidi ya timu bora sana ambayo haikumudu kupiga hata shuti moja liliolenga goli.”
United wameshinda mechi mbili tu kati ya tisa za mwisho walizocheza Ligi Kuu Uingereza.