Follow

Cristiano Ronaldo apata shavu kucheza Ligi ya China

Je! Ni wakati sahihi kwa Cristiano Ronaldo kucheza ligi ya China kama Tevez, Oscar na wanasoka wengine maarufu dunaini?
Real Madrid wamepewa dau la paundi milioni 256.6 na klabu ya China ambayo haijawekwa bayana kwa ajili ya Cristiano Ronaldo, kwa mujibu wa wakala wa mshambulizi huyo Jorge Mendes.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno, hivi karibuni alitwaa tuzo ya Ballon d’Or kwa mara ya nne, na inasemekana pia kwamba ametengewa kitita cha paundi milioni 85 kama ujira wake kwa mwaka ili ajiunge na klabu hiyo.
Medes amedai kuwa Ronaldo ameitosa fursa hiyo, hiyo ni baada ya kutangaza nia yake kuendelea kubaki Bernabeu kipindi chake chote cha soka kilichobakia.
Akiongea na Sky Sports Italia, Medes alisema: “kutoka China wameitengea Real Madrid dau la euro milioni 300 na zaidi ya euro milioni 100 kwa mwaka kwa ajili ya mchezaji. Lakini fedha si kila kitu. Real Madrid ni maisha yake. Cristiano Ronaldo yupo Real Madrid na haiwezekani kwenda China.
“Soko la kichina ni soko jipya. Wanaweza kununua lundo la wachezaji, lakini haiwezekani kwa Ronaldo kwenda huko. Cristiano ni mchezaji bora na mahiri zaidi duniani, hajawahi kutokea kama yeye. Ni jambo la kawaida kupokea ofa kadhaa.
“Ametwaa Ubingwa wa Bara Ulaya akiwa na Ureno, ni kama kushinda ligi ya Italia na Genoa – hawakupewa nafasi kubwa kushinda.”
Shanghai Shenhua imetangaza Alhamisi kuwa mchezaji wa zamani wa Manchester United na Manchester City Carlos Tevez amejiunga na klabu hiyo akitokea Boca Juniors, akiongeza orodha ya wachezaji wakubwa waliotimkia kwenye nchi hiyo ya Mashariki ya Mbali miaka ya hivi karibuni.
Instagram Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment

picture of the week

picture of the week

NI LIVERPOOL DHIDI YA WTAKATIFU MANE KUKUTANA NA TIMU YAKE KWA MARA YA KWANZA

NI LIVERPOOL DHIDI YA WTAKATIFU MANE KUKUTANA NA TIMU YAKE KWA MARA YA KWANZA