Follow

Guardiola hajavutiwa na mbinu za Boro

Aguero na De Bruyne walipoteza nafasi nyingi jambo ambalo kocha wa Manchester City Pep Guardiola alionesha kutofurahishwa nalo
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amesema kuwa hakufurahishwa na mbinu zilizotumiwa na Middlesbrough katika mechi yao ya Ligi Kuu Uingereza iliyochezwa Jumapili.
City walipoteza pointi za thamani kwao katika mbio za taji Ligi Kuu baada ya Moten De Roon kufunga goli la kusawazisha katika dakika za majeruhi na kulifanya goli la Sergio Aguero kutokuwa na maana katika uwanja wa Etihad.
Aguero na Kevin De Bruyne walikosa nafasi nyingi ambazo zingeweza kuwapa wenyeji wa mechi hiyo ushindi na Guardiola alionyesha kukasirishwa kwa nafasi hizo zilizopotea.
Simon Msuva mchezaji Bora Ligi Kuu mwezi Oktoba
Alipoulizwa kama alivutiwa na mbinu za mipango ya Boro, Guardiola alisema: “Hapana, sijavutiwa… Sipo hapa kuzungumzia kiwango cha wapinzani wangu. [Aito Karanka] ndiye kocha wao na anajua vema kuliko mimi jinsi gani wanataka kucheza. Kipindi cha pili hatukucheza kama ilivyokuwa kipindi cha kwanza lakini sidhani kama tulicheza vibaya.
“Nadhani walipata nafasi moja mwanzoni mwa kipindi cha pili na nyingine dakika ya mwisho. Kama ilivyokuwa dhidi ya Everton na Southampton, unapoona kile wapinzani walichofanya katika mechi zote tatu tukiwa nyumbani na tumepoteza pointi sita, wameingia kama mara nne au tano ndani ya eneo letu la boksi. Walikuwa na wachezaji 10 ndani ya boksi dakika 90, haikuwa kazi rahisi kwetu.
“Tulitengeneza nafasi za kutosha, tulishambulia vizuri na tulifanya mashambulizi ya kushtukiza, lakini unapofika dakika za mwisho ukiwa unaongoza kwa 1-0 lolote laweza kutokea. Kama tukizungumzia ustadi baada ya mechi ngumu Jumanne iliyopita, namna tulivyoanza, kuupeleka mpira kulia na kushoto, yawezekana dakika za mwisho timu ilichoka. Lakini kama tungefunga goli kwa kupitia nafasi za Sergio Aguero au Kevin (De Bruyne), mchezo ungekuwa umekwisha.”
City sasa wamecheza bila ushindi katika mechi zao tatu za mwisho za nyumbani na wameshinda mechi moja tu kati ya tano za mwisho Ligi Kuu.
Instagram Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment

picture of the week

picture of the week

NI LIVERPOOL DHIDI YA WTAKATIFU MANE KUKUTANA NA TIMU YAKE KWA MARA YA KWANZA

NI LIVERPOOL DHIDI YA WTAKATIFU MANE KUKUTANA NA TIMU YAKE KWA MARA YA KWANZA