Follow

El Clasico: Nani atashinda Barcelona au Real Madrid? Somba uchambuzi hap

Real Madrid imeshinda mechi 93 na magoli 391 huku Barcelona ikiwa imeshinda mechi 91 na magoli 379 katika mechi walizokutana, Nani atashinda J'mosi?
Hakuna kinachoweza kulinganishwa na mechi baina ya miamba hawa wawili – wakati baadhi ya mechi kubwa zinaweza kugawa miji au hata nchi, Barcelona na Real Madrid zenye mashabiki wengi duniani zina kila sababu ya kuugawa ulimwengu kufuatia mvuto mkubwa wa mechi ya El Clasico.
Real Madrid wapo kileleni kwa tofauti ya pointi sita La Liga, kikosi hicho cha Zinedine Zidane kimekuwa na wakati mzuri tangu kuanza kwa msimu huu kwani bado hawajapoteza mchezo, na mwendo huo ni mwendelezo wa kutokea Februari msimu uliopita (mechi 25 tangu walipofungwa mara ya mwisho).
Hata hivyo, mashabiki wa Barcelona watakumbuka mwendelezo wa mechi 39 mfululizo, zenye ushindani mkubwa bila kufungwa kabla ya El Clasico ya mwisho na jinsi walivyofungwa katika uwanja wa Camp Nou – Hii inamaanisha jambo hilo linaweza kuwapata wapinzani wao awamu hii.
Mechi walizokutana:
Jumla ya mechi rasmi inatofautiana kwa moja iwapo unataka kuhesabu nusu fainali ya 1902 Copa de la Coronacion kama moja ya mechi rasmi – tofauti na Kombe la FA la Hispania; mechi ya kwanza rasmi ya Clasico Barcelona walishinda 1-3 ugenini.
Real Madrid wapo mbele kwa idadi ya ushindi – mechi 93 ikilinganishwa na 91 za Blaugrana. Barcelona imepoteza mechi tatu kati ya 13 za Clasico walizocheza nyumbani katika michuano yote (Ushindi 7, Sare 3).
Real Madrid wameshinda mechi tano kati ya tisa walizaocheza dhidi ya Barca katika michuano yote (wakifungwa nne), ikiwa ni pamoja na ziara yao ya mwisho Camp Nou (1-2).
Takwimu muhimu:
  • Iwapo Barcelona watashinda mechi hii, utakuwa ni ushindi wao wa 50 dhidi ya Real Madrid katika uwanja wa nyumbani kwenye mechi za La Liga.
  • Barcelona wamefunga katika kila mechi kati ya mechi zao 21 dhidi ya Real Madrid, mwendo mzuri wa timu hiyo katika historia ya Clasico (michuano yote).
  • Lionel Messi ndiye kinara wa kupachika mabao katika mechi za Clasico akiwa na magoli 21.
  • Alfredo Di Stefano pekee (18) ndiye aliyefunga magoli mengi Real Madrid kuliko Cristiano Ronaldo (16) kwenye mechi za Clasico katika michuano yote.
  • Neymar amehusika kwenye magoli matano katika mechi sita za Clasico (magoli matatu na pasi mbili za mwisho).
  • Karim Benzema amefunga magoli matano katika mechi saba za mwisho za Clasico La Liga, lakini moja tu lilipatikana katika uwanja wa Camp Nou.
Habari za Timu – Barcelona 
Wachezaji wawili wapo shakani katika kikosi cha Barcelona – wakati Mathieu yupo nje kabisa, Iniesta na Jordi Alba ndio wachezaji wanaongaliwa kwa umakini zaidi, ingawa wote hawana uhakika wa kucheza mechi hii, lakini uhitaji unaweza kumlazimu Luis Enriquekuwatumia itakapobidi.
Andres Iniesta ameripotiwa kuwa tayari kucheza sehemu ya mechi, kwa hiyo bado imebaki kitendawaili iwapo ataanza au ataingia kutokea benchi.
Pique na Mascherano wataongoza safu ya ulinzi kwa timu ya nyumbani, wakati utatu wa Barca MSN utafanya jukumu lao la mashambulizi kama kawaida.
Habari za Timu – Real Madrid
Gareth Bale ndiye mchezaji muhimu anayekosekana kwenye kikosi cha Madrid, pamoja na Toni Kroos. Wawili hao nafasi zao zitachukuliwa na Lucas Vazquez na Mateo Kovacicmtawalia, wakati nafasi ya tatu katika safu ya kiungo (pembeni mwa Luka Modric) itatwaliwa na Casemiro ambaye anaonekana kuwa na afya njema kwa mchezo huo.
Pepe atashirikiana na Ramos katika beki ya kati na Carvajal na Marcelo wakicheza pembeni.

Instagram Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment

picture of the week

picture of the week

NI LIVERPOOL DHIDI YA WTAKATIFU MANE KUKUTANA NA TIMU YAKE KWA MARA YA KWANZA

NI LIVERPOOL DHIDI YA WTAKATIFU MANE KUKUTANA NA TIMU YAKE KWA MARA YA KWANZA