Follow

OZIL NAE KIGEUGEU "NATAMANI KURUDI MADRID"

Nyota wa Arsenal Mesut Ozil anajuta kuondoka Real Madrid, na bado hajafunga milango kurudi kwenye klabu hiyo ya Hispania kwa mujibu wa habari
Kiungo huyo wa Ujerumani aliihama klabu hiyo ya Hispania kujiunga na Arsenal 2013 kwa kiasi cha paundi milioni 42.5 na baada ya mwanzo wa wastani sasa amekuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Arsene Wenger.
Mjerumani huyo ambaye ni mshindi pia wa Kombe la Dunia yupo kwenye mazungumzo na klabu ya Arsenal kuhusu mkataba mpya lakini bado maafikiano ya mkataba mpya hayajafikiwa, kama ilivyo kwa Alexis Sanchez.
Kwa mujibu wa Marca, Ozil anajuta kuondoka Real Madrid na angependa kurudi Santiago Bernabeu, ambapo alitwaa mataji matatu ikiwa ni pamoja na La Liga kampeni za 2011-12.
Nyota huyo, 28, ambaye mkataba wake unafika kikomo 2018 anaaminika kuwa mfuasi mkubwa wa rais wa Real Florentino Perez.
Ozil amekuwa mchezaji mwenye ushawishi mkubwa kwa Washika Mtutu msimu huu, na amefunga mabao saba katika michuano yote.
Granit Xhaka: “Mesut Ozil ana ubora wa kipekee”
Kiungo wa Arsenal Granit Xhaka amemwelezea mchezaji mwenzake Mesut Ozil kama moja ya wachezaji bora duniani.
Xhaka waliungana na Ozil kucheza kikosi kimoja Arsenal majira ya joto lakini tayari amekiri kuguswa na uwezo wa kiungo huyo wa Kijerumani, ambaye amefunga magoli saba katika mechi kumi na saba alizocheza akiwa na Gunners msimu huu.
Xhaka aliliambia gazeti maarufu la Ujerumani, Bild: “Mesut Ozil ana ubora ambao mimi binafsi sijawahi kuona hapo awali.
“Anafanya miujiza mikubwa kwa mguu wake wa kushoto, ana kasi – hata inapokuwa tofauti wakati mwingine, na yu miongoni mwa wachezaji bora duniani.”
Xhaka aliigharimu Arsenal ada ya uhamisho ya paundi milioni 35 majira ya joto – milioni 7.5 pungufu ya ile waliyolipa kumsajili Ozil 2013.
Instagram Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment

picture of the week

picture of the week

NI LIVERPOOL DHIDI YA WTAKATIFU MANE KUKUTANA NA TIMU YAKE KWA MARA YA KWANZA

NI LIVERPOOL DHIDI YA WTAKATIFU MANE KUKUTANA NA TIMU YAKE KWA MARA YA KWANZA