Follow

Majanga: Nyota mwingine Manchester United kukosa mechi saba kwa majeraha

Manchester United imeendelea kuandamwa na majanga baada ya nyota mwingine kupata majeraha yatakayomkosesha mechi saba
Smalling ambaye hivi karibuni ameonekana kutokuwa chaguo hasa la Jose Mourinho alivunja kidole gumba chake mazoezini mapema wiki hii na anatazamiwa kukosa mechi saba zijazo zaManchester United.
Habari za majeraha ya Smalling bila shaka si habari mbaya sana kwa Jose Mourinho ambaye tayari amemkosa beki chaguo la kwanza Eric Bailly huku Phil Jones na Marcus Rojo wakiwa kama mbadala katika safu ya mabeki wa kati, lakini huenda akalazimika kusajili beki mwingine wa kati katika dirisha la uhamisho wa Januari.
Siyo siri kwamba Jose Mourinho anataka kuimarisha safu yake ya beki majira ya joto na ukizingatia kuaw Smalling na Bailly watakosekana kwa muda kidogo, Mreno huyo anaweza kuanza kumfuatilia Virgil Van Dijk wa Southampton.
Mdachi huyo amekuwa katika kiwango bomba kwa Southampton msimu huu na ingawa Saints wakihaha kumbakisha nyota wao huyo kama Goal inavyoelewa, watakuwa tayari kumuuza beki huyo kama wakipokea ofa nono.
Uwezo mzuri wa Van Dijk katika kukaba kadhalika na kuweza kuusoma mchezo, vinamfanya kuwa moja ya mabeki hatari zadi katika bara la Ulaya, na bila shaka ni mchezaji anayeweza kuimarisha safu ya mabeki.
Ili Mourinho aweze kupindua matokeo katika Old Trafford anahitaji wacheza ambao wanaweza kubadili mchezo na kuleta matokeo mazuri hata katika mazingira magumu na inawezekana Van Dijk ndiye mchezaji anayeweza kufanya kazi hiyo.
Haitakuwa kazi rahisi kumwondoa Van Dijk mikononi mwa Southampton lakini Mourinho ni lazima aweze kumshawishi Mdachi huyo kutua Old Trafford dirisha la uhamisho wa Januari ili aweze kutatua tatizo la safu ya ulinzi ya timu yake.
Instagram Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment

picture of the week

picture of the week

NI LIVERPOOL DHIDI YA WTAKATIFU MANE KUKUTANA NA TIMU YAKE KWA MARA YA KWANZA

NI LIVERPOOL DHIDI YA WTAKATIFU MANE KUKUTANA NA TIMU YAKE KWA MARA YA KWANZA