Follow

Lukaku amfikia Harry Kane mbio za kiatu cha dhahabu

Kane na Lukaku kwa sasa wapo kwenye vita ya kuwania kiatu cha dhahabu, kadhalika na Alexis Sanchez, Diego Costa, Zlatan Ibrahimovic na Defoe
Romelu Lukaku alifikia idadi ya mabao ya Harry Kane katika mbio za kiatu cha dhahabu Ligi Kuu Uingereza Everton ilipong'ara dhidi ya West Brom kwa kupata ushindi wa tano mfululizo nyumbani.
Mbelgiji huyo alifunga baada ya magoli ya kipindi cha kwanza kutoka kwa Kevin Mirallas na Morgan Schneiderlin Everton ikiibuka na ushindi wa 3-0 Jumamosi.
Lukaku alipata fursa ya kufikia idadi ya mabao ya Kane, huku Manchester City, Manchester United, Arsenal, Chelsea na Tottenham zikicheza mechi za Kombe la FA wikiendi hii hatua ya robo fainali.
Kane alishika usukani katika mbio za kiatu cha dhahabu wikiendi iliyopita dhidi ya Everton ya Lukaku, kwa kufunga magoli mawili kuipa timu yake ushindi wa 3-2 licha ya goli la dakika za jioni kutoka kwa Lukaku.
Kane na Lukaku kwa sasa wapo kwenye vita ya kuwania kiatu cha dhahabu, kadhalika na Alexis Sanchez, Diego Costa, Zlatan Ibrahimovic, Defoe, Dele Alli, Sadio Mane, Aguero na Hazard.
Hata hivyo, Lukaku alisema awali kabla ya kipigo dhidi ya Spurs kwamba hana lengo la kutaka kuweka rekodi.
"Sitaki kuangalia nini wanafanya wachezaji wengine," alisema Lukaku. "Hilo ndilo lililoninyima kiatu cha dhahabu mwaka jana, kwa hiyo kwangu mimi cha muhimu ni kupata ushindi tu.
"Muhimu ni kushinda mechi nyingi iwezekanavyo na kufunga mabao mengi pia."
Instagram Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment

picture of the week

picture of the week

NI LIVERPOOL DHIDI YA WTAKATIFU MANE KUKUTANA NA TIMU YAKE KWA MARA YA KWANZA

NI LIVERPOOL DHIDI YA WTAKATIFU MANE KUKUTANA NA TIMU YAKE KWA MARA YA KWANZA