Follow

Matukio yalikuwa gumzo katika soka la Tanzania kwa kipindi cha miezi 12

2016 ni miongoni mwa miaka ambayo haitasahulika katika mpira wa hapa nchini maana uliambatana na matukio mengi yenye furaha na udhuni pia
Matukio mengi yametokea kwenye mpira wa Tanzania kwenye kipindi cha miezi 12 nyuma, ndani ya mwaka nzima tumeshuhudia timu yetu ya taifa ikizidi kuporomoka kila kukicha huku majirani zetu Uganda wakipiga hatua moja mbele baada ya kufuzu michuano ya afrika AFCON nchini Gabon
Pia 2016 ni mwaka ambao una neema kwa soka letu kwa kushuhudia baadhi nyota wakipata nafasi ya kusakata kabumbu kwenye nchi zilizo piga hatua, Mbwana Samatta ndiye aliyekuwa wa kwanza kufungua milango kwa kusaini na klabu ya Genk ya Ubelgiji na hivi karibuni Farid Mussa naye amefanikiwa kwenda kujiunga na Teneriffe ya Hispania inayo shiriki daraja la pili
Goal inakuletea matukio 11 yaliyo kuwa gumzo mwaka 2016 katika soka la tanzania
1.Mbwana Samatta anyakuwa tuzo ya mchezaji bora Afrika kwa wachezaji wanao cheza Afrika pekee Januari 7
Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu kutoa mchezaji bora Afrika, Samatta alitwaa tuzo hio ziilizo fanyika nchini Nigeria Januari 7 2016 baada ya kuwabwaga wachezaji kama kidiaba walio kuwa na mafanikio lukuki kwa kipindi hicho
2.Kashfa ya upangaji matokeo daraja la pili
Mwishoni mwa mwezi wa pili kuli ibuka na skendo ya upangaji wa matokeo daraja la pili ambayo ilikuja kuichafua Shirikisho la mpira Tanzania TFF, tukio hili lilileta mvutano nchini, katika kashfa hii ilipelekea timu za JKT Orjoro, Geita Gold, Polisi Tabora na JKT Kanembwa kushushwa madaraja ya chini pia baadhi ya wachezaji kukumbwa na rungu la kufungiwa maisha
3.Klabu ya Yanga kunyakuwa mataji yote ya ndani
2016 ni mwaka wenye mafanikio kwa klabu ya Yanga, katika miezi hiyo 12 wana Jangwani walifanikiwa kuweka mataji yote yaliyo chini ya chama cha mpira , taji la Shirikisho fa na  taji la Ligi Kuu
4.Yanga wafuzu hatua ya makundi Shirikisho Afrika baada ya miaka 18
Wana Jangwani wana fanikiwa kuitoa sagrada esperanca ya angola na kufuzu robo fainali Shirikisho Afrika baada ya miaka 18, chini ya Mholanzi Hans vijana hawa wanapata nafasi hio japo hawakufanya vizuri hatua ya makundi
5.Dhana ya mabadiliko kwenye klabu za Simba na Yanga yavuta kasi mwaka 2016
Dhana ya mabadiliko ndani ya klabu hizi kongwe ilikuwa ndiyo mjadala mkubwa kwa mwaka 2016, klabu zote zimeonesha nia ya kutaka kuachana na mfumo wa zamani na kuamia kwenye mifumo ya kisasa
6.Twiga Stars bingwa wa Cecafa 
Timu ya soka ya wanawake waibuka mashujaa kwa Taifa, Twiga Stars wafanikiwa kuwa mabingwa wa kombe la Cecafa lililofanyika nchini Uganda, wana dada hao walifanikiwa kushinda taji hilo baada ya kuifumua timu ya taifa ya Kenya kwa magoli mawili kwa moja
7.Serikali yazivungia Simba na Yanga kutumia Uwanja wa Taifa
Kwenye mechi ya watani wa jadi iliyo fanyika tarehe moja mwezi wa kumi, kulitokea uharibifu wa vifaa vya uwanja na kupelekea waziri mwenye zamana Nape Nnauye kuvipiga marufuku klabu hizi kongwe kutumia Uwanja wa Taifa
8.Sakata la usajili wa Ramadhani Kessy kwenda Yanga
Bado kuna hali ya sintofahamu kwenye usajilli wa Kessy kutoka Simba kwenda Yanga, usajili huu ndiyo ulikuwa gumzo kwa mwaka 2016 hasa kutokana sinema nyingi katika ishu hii
9.Wachezaji wa Yanga wagomea mazoezi
Hili ni tukio la hivi karibuni, wachezaji wa klabu ya Yanga kugomea mazoezi ya siku mbili wakishinikiza viongozi  wawalipe mishahara na posho zao za mwezi wa kumi na moja
10.Kifo cha mchezaji wa Mbao U-20
Ni tukio lililo gusa hisia za watu wengi wa soka kwa mwaka 2016, Ismail Mrisho mchezaji wa Mbao U-20 alianguka ghafla na kupoteza maisha uwanjani kwenye mchezo dhidi ya Mwadui
11.Simba yafunga mwaka kileleni baada ya miaka 4
Mwaka huu umeisha vizuri kwa wana Msimbazi wote kwani wamefanikiwa kumaliza mwaka wakiwa kileleni, hii ni mara ya kwanza baada ya takribani miaka 4 kuwahi fanya hivyo
Instagram Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment

picture of the week

picture of the week

NI LIVERPOOL DHIDI YA WTAKATIFU MANE KUKUTANA NA TIMU YAKE KWA MARA YA KWANZA

NI LIVERPOOL DHIDI YA WTAKATIFU MANE KUKUTANA NA TIMU YAKE KWA MARA YA KWANZA