Uganda The Cranes wamejipatia ushindi wa kwanza katika mbio za kufuzu Kombe la Dunia la Fifa 2018 baada ya kuwafunga Mashetani Wekundu Jumamosi
Uganda waliigeuza presha kwa Ghana kwa kuifunga Congo nyumbani katika mechi ya Jumamosi Kundi E mjini Kampala.
Farouk Miya ndiye aliyekwamisha wavuni mpira na kuwapatia Cranes ushindi wa 1-0 uliowapandisha hadi kileleni mwa kundi E, wakati Mashetani Wekundu wakibakia mkiani.
Milutin Sredojevic alilazimika kumwanzisha kipa mzoefu na tegemeo lao Dennis Onyangokatika moja ya mabadiliko matatu aliyofanya kwenye kikosi kilichowashika Black Stars katika sare tasa mwezi uliopita.
Hata hivyo kikosi hicho cha Sredojevic kilipata pigo ikiwa ni baada tu ya dakika nane za mchezo baada ya Murshid Jjuuko kugongana na mpinzani wake na kulazimika kubadilishwa mara moja.
Lakini Miya alifanya kazi maridadi kabisa ya kuwapatia Uganda goli la kuongoza dakika ya 18 ambalo pia lilidumu hadi dakika ya mwisho ya mechi hiyo hivyo kuifanya timu yake kuongoza kundi kabla ya mechi ya Ghana na Misri itakayopigwa Jumapili.
Matokeo hayo yameigeuzia presha kwa Ghana inayonolewa na Avram Grant kuelekea kwenye mechi kali, ngumu na inayosubiriwa kwa hamu na walio wengi dhidi ya Mafarao katika uwanja wa Borg El Arab Jumapili jioni.
Katika kiwango safi kabisa Uganda waliishikilia Ghana kwa sare ya 0-0 katika Tamale mwezi uliopita, matokea ambayo kwa yakini yanaigharimu kwani ilikuwa mechi yao ya ufunguzi nyumbani wakati vijana wa Hector Cuper tayari wanashikilia pointi tatu baada ya kuifunga Congo katika mechi yao ya ufunguzi mwezi uliopita.
Misri wana nafasi kubwa kushinda dhidi ya Ghana wanapocheza nyumbani kwani Ghana wamewafunga mara mbili tu kati ya mechi kumi na moja ambazo wamecheza dhidi ya nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika .
Mara ya mwisho timu hizo kukutana ilikuwa 2014 Kufuzu Kombe la Dunia ambapo Ghana waliikung’uta Misri 6-1 raundi ya kwanza wakati Misri wakijibu mapigo kwa ushindi wa 2-1 mechi ya marudiano.
Ghana watalazimika kushinda mechi ya Jumapili kufufua tumaini lao la kufuzu kwani ushindi kwa Misri utawaweka pabaya kwenye kundi lao.


0 comments:
Post a Comment