Follow

Watakaopigania tuzo ya mwanasoka bora zaidi Afrika 2016

Wachezaji watano watakaoshindania Tuzo ya BBC ya Mwanakandanda Bora wa Afrika wa Mwaka 2016 wametangazwa.
Wachezaji hao ni Pierre-Emerick Aubameyang, Andre Ayew, Riyad Mahrez, Sadio Mane and Yaya Toure.
Wachezaji hao watano walitangazwa wakati wa kipindi maalum cha moja kwa moja runingani Jumamosi.
Mshindi atachaguliwa na mashabiki wa soka ya Afrika kutoka kila kona ya dunia. Mashabiki wana hadi saa 18:00 GMT tarehe 28 Novemba kumpigia kura mchezaji wanayempenda.
Mnamo Jumatatu, 12 Desemba, mshindi wa tuzo hiyo atatangazwa moja kwa moja kwenye runinga ya BBC Focus on Africa pamoja na redio, kuanzia saa 17:35.
Tovuti za BBC SwahiliBBC Sport na BBC Africa pia zitachapisha habari za mshindi.


Aubameyang ameorodheshwa kwa mwaka wan ne mtawalia, mshindi wa mwaka 2011 pia ameorodheshwa kwa mwaka wa nne, Mahrez ndiye mchezaji pekee ambaye hajawahi kuorodheshwa kushindania, Mane alishindania mara ya kwanza mwaka jana naye mshindi mara mbili. Toure ameorodheshwa kwa mwaka wa nane mtawalia.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Gabon Aubameyang amekuwa na kipindi cha kufana sana mwaka 2016, amefunga mabao 26 (kufikia wakati wa kuandika makala hii) katika klabu yake ya Borussia Dortmund nchini Ujerumani
Alikuwa mchezaji wa kwanza kutoka Afrika kutawazwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwaka wa Bundesliga, raia wa kwanza wa Gabon kushinda Tuzo ya Shirikisho la Soka Afrika ya mchezaji bora wa mwaka Afrika, na ameorodheshwa miongoni mwa wachezaji wanaoshindania tuzo ya mchezaji bora duniani mwaka 2016, tuzo ya Ballon d'Or
Instagram Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment

picture of the week

picture of the week

NI LIVERPOOL DHIDI YA WTAKATIFU MANE KUKUTANA NA TIMU YAKE KWA MARA YA KWANZA

NI LIVERPOOL DHIDI YA WTAKATIFU MANE KUKUTANA NA TIMU YAKE KWA MARA YA KWANZA