Follow

Breaking: Ngassa mbioni kujiunga Mbeya City

Hii itakua ni mara ya pili kwa Ngassa kusainiwa na kocha Kinnah Phiri mara ya kwanza ikiwa ni alipomsajili Free State ya Afrika Kusini
Hatimaye mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Yanga na timu ya taifa ya Tanzania Mrisho Ngasa amerejea nchini na kujiunga na Mbeya City.
Msemaji wa timu hiyo Dismasi Ten ameiambia Goal, mazungumzo yao na Ngassa yamekamilika na muda wowote wataweka mambo hadharani baada ya kumaliza taratibu zote za usajili.
“Ni kweli tulikuwa kwenye mazungumzo ya muda mrefu na Ngassa na kwa sasa siwezi kusema chochote lakini baada ya siku mbili tutazungumza jambo kwa watu wa soka kuelewa nini kinachoendelea kati yetu na Nagassa,”amesema Ten.
Msemaji huyo amesema Ngassa anamapenzi makubwa na Mbeya City na kabla ya kwenda Oman alikwenda Mbeya na kuzungumza na kocha wao Kinnah Phiri ambaye ni rafiki yake mkubwa kitu ambacho kiliwapa uhakika wa kuinasa saini ya mchezaji huyo.
Amesema mchezaji huyo hajapendezwa na maisha ya Omon alipokuwa anaichezea klabu ya Fanja, na ndiyo maana yupo nchini akisaka timu ya kucheza na wao wapo kwenye mazungumzo naye wakiamini anaweza kuwa msaada kwao kwenye mzunguko wa pili.
“Unajua Ngassa ni mchezaji mwenye rekodi ya kipekee hapa nchini kwanza anauzoefu mkubwa hakuna timu ambayo inaweza kumkataa kutokana na kipaji alichokuwa nacho ndiyo maana nasema kama mambo yakienda sawa anaweza kuwa mchezaji wetu.,”amesema Ten.
Wakati hayo yakiendelea tayari msemaji wa timu hiyo ameposti picha akipeana mikono na Ngassa kwa furaha baada ya kukamilisha baaadhi ya mambo ambayo inadaiwa ni makubaliano ya kusaini mkataba.
Kama kweli Ngassa atasaini fomu za kuichezea Mbeya City itakuwa ni mara ya pili kwa kocha Kinnha Phiri kuungana na winga huyo hatari Afrika Mashariki kufanya kazi na mchezaji huyo mara ya kwanza wawili hao kufanya kazi pamoja ilikuwa ni Free State ya Afrika Kusini ambapo kocha huyo Mmalawi alimsajili kutoka Y
Instagram Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment

picture of the week

picture of the week

NI LIVERPOOL DHIDI YA WTAKATIFU MANE KUKUTANA NA TIMU YAKE KWA MARA YA KWANZA

NI LIVERPOOL DHIDI YA WTAKATIFU MANE KUKUTANA NA TIMU YAKE KWA MARA YA KWANZA