Follow

Ni wakati wa Mourinho kumsajili Antoine Griezmann

Jana ilishuhudiwa Manchester United ikienda sare ya tano msimu huu ikiwa ni ndani ya meche saba za ligi kuu za hivi karibuni baada ya mchezo wao dhidi ya West Ham United kumalizika kwa matokeo ya 1-1 kwenye uwanja wa Old Trafford.
Licha ya kutengeneza nafasi zipatazo kumi na saba huku mashuti nane yakilenga lango la wapinzani lakini Manchester United ilishindwa kuibuka na pointi tatu kwenye uwanja wake wa nyumbani.
Hii sio mara ya kwanza tungu kuanza kwa msimu huu 2016/17  ligi kuu nchini England kushuhudia United ikicheza vizuri na kutawala mchezo lakini ikishindwa kupata matokeo. Imetokea dhidi ya michezo dhidi ya Burley, Stoke City na Arsenal huku tatizo kubwa likiwa ni kukosa umakini kwa safu yake ya Ushambuliaji.
United wanatengeneza nafasi nyingi lakini wamekuwa wakitumia chache kupachika mabao. Jambo ambalo liwewafanya hadi sasa kuwepo nafasi ya sita wakiwa na pointi 20 ikiwa ni ishara ya mwendo wa kusuasua ukilinganisha na timu za Chelsea, Liverpool, Man City na Arsenal ambazo zimekuwa zikifunga mabao na kukusanya pointi za kutosha.
Man United inahitaji mshambuliaji kwenye dirisha dogo la usajili mwezi Januari mwenye uwezo wa kuja kumalizia nafasi zinazotengenezwa na United. Hata kama itampata Griezmann kutoka Atletico Madrid kama zinavyosema tetesi za usajili za dirisha dogo la Januari anaaweza kuisaidia Man United kwenye tatizo ambalo limekuwa likiwasumbua kwa siku za karibuni.
Instagram Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment

picture of the week

picture of the week

NI LIVERPOOL DHIDI YA WTAKATIFU MANE KUKUTANA NA TIMU YAKE KWA MARA YA KWANZA

NI LIVERPOOL DHIDI YA WTAKATIFU MANE KUKUTANA NA TIMU YAKE KWA MARA YA KWANZA