Follow

Agyei amesaini mkataba wa miaka mitatu Azam FC kazi kuanza Januari

Kawemba amesema mbali na kumsaini mchezaji huyo pia wanatarajia kuwafanyia majaribio wachezaji saba wapya kutoka mataifa mengine
Klabu ya Azam imekamilisha usajili wa winga chipukizi raia wa Ghana, Enock Atta Agyei kutokaMedeama ambaye ataanza kuitumikia timu hiyo mzunguko wa pili utakapoanza.
Mtendaji mkuu wa klabu ya Azam Saad Kawemba, ameiambia Goal, wamemsajili mchezaji huyo kwa mkataba wa miaka mitatu na hiyo ni baada ya kufikisha umri wa miaka 18 ambao kwa sheria za nchini kwao zinamruhusu kufanya kazi nje ya nchi.
“Ni kweli Agyei, tumempa mkataba wa miaka mitatu kama mtakumbuka mwezi Septemba tulimsajili kutoka kwenye klabu yake ya Medeama ya Ghana, lakini alishindwa kufanya kazi na sisi kwa sababu alikuwa na umri wa miaka 17, kwa sheria za Ghana zilikuwa hazimruhusu kufanya kazi nje ya taifa lao lakini sasa ametimiza miaka 18 na ndiyo maana amekuja na sisi tumemuongeza mwaka moja baada ya miwili tuliyompa awali,” alisema Kawemba.
Kawemba amesema mbali na kumsaini mchezaji huyo pia wanatarajia kuwafanyia majaribio wachezaji saba wapya kutoka mataifa mengine.
“Tumewapokea wachezaji saba kwa ajili ya majaribio wachezaji hao ni Mbimbe Aaron Nkot (Cameroon), Kone Nabil Ibrahim (Ivory Coast), kiungo mkabaji Kingue Mpondo Stephane (Cameroon),Yaya Awaba Joel (Cameroon), Samuel Afful, Benard Ofori (wote Ghana) na Konan Oussou kutoka Ivory Coast,” amesema Kawemba. 
Kiongozi huyo amesema wanataka kurudi kwa kasi kwenye mzunguko wa pili na kurudi kwenye mbio za ubingwa wa ligi ya Vodacom baada ya kuanza vibaya msimu huu.
Amesema anaimani kocha wao Zeben Hernandez, atatumia vizuri taaluma yake kwa kufanya uteuzi mzuri ambao utakuwa na tija kwa timu hiyo hasa ukizingatia wanakwenda kwenye duru la lala salama la ligi ya Vodacom na michuayo ya Kombe la Shirikisho Afrika ambalo wanatarajia kushiriki mwezi Januari.
Instagram Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment

picture of the week

picture of the week

NI LIVERPOOL DHIDI YA WTAKATIFU MANE KUKUTANA NA TIMU YAKE KWA MARA YA KWANZA

NI LIVERPOOL DHIDI YA WTAKATIFU MANE KUKUTANA NA TIMU YAKE KWA MARA YA KWANZA