Mambo yanaonekana kwenda mrama kwa Mkhitaryan kwani hapati kile alichokitarajia katika kikosi cha United chini ya Jose Mourinho na huenda akarudi BVB
Mkhitaryan ameanza mechi moja tu Ligi Kuu Uingereza tangu alipotua Old Trafford akitokea BVB majira ya joto.
Na klabu hiyo ya Bundesliga imejipanga kumchukua tena nyota huyo wa kimataifa wa Armenia kwa mkopo mwaka mpya utakapoanza.
Cruyff: "Depay anahitaji dakika zaidi Manchester United"
Kiungo wa zamani wa Manchester United Jordi Cruyff amesema kuwa winga anayehaha Memphis Depay anahitaji kupewa muda zaidi wa kucheza.
Depay aliwasili Manchester United mwaka jana baada ya muda mrefu kuzungumziwa kama mchezaji bora duniani kwa siku zijazo, lakini ameshindwa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza United licha ya klabu kuendelea chini ya utawala wa makocha wawili katika kipindi chake kwenye Ligi Kuu Uingereza.
Cruyff, ambaye alidumu misimu minne Old Trafford, haamini kama amali ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ndio imeishia hapo United, lakini, badala yake amesema Jose Mourinho anahitaji kumpa mchezaji huyo kinda fursa ya dakika zaidi kucheza dimbani ili kumsaidia kuendeleza kipaji chake.
“Kwa hakika, United ni klabu kubwa na yenye mafanikio, lakini nadhani pia Depay ni mchezaji mahiri,” Cruyff alikiambia Gulf News.
“Kitakwimu, hapati muda wa kutosha dimbani, lakini sijui muda anaoingia mchezoni na kutoka. Lakini kwa hakika, ana uwezo mkubwa na ameonesha hilo.
“Sasa mbinu ni kuhakikisha anapata fursa ya kucheza japo kila wiki. Hatimaye atakuwa bora zaidi, lakini haijulikani ni wapi na lini.”
Depay amecheza mechi 33 Manchester United, akifunga mabao mawili katika mechi hizo.


0 comments:
Post a Comment