Mkali Victor Moses ndiye aliyefungua na kufunga jeneza la Algeria Nigeria wakiwazika waarabu kwa ushindi wa mabao 3-1 Jumamosi
Victor Moses alifungua na kufunga ubao wa magoli Nigeria wakiinyuka Algeria 3-1 Jumamosi kuongoza kundi lao katika mbio za kufunzu Kombe la Dunia 2018.
Nahodha John Obi Mikel, mchezaji mwenza wa Moses katika klabu ya Chelsea pia alikuwa katika kiwango cha hali ya juu kwenye kikosi cha Nigeria katika uwanja wa Uyo wakati Nabil Bentaleb akiipatia Algeria goli la ufundi wa hali ya juu.
Jambo la kushangaza kabisa Cameroon ikishikiliwa kwa sare ya 1-1 nyumbani na Zambia, Nigeria imeweza kuongoza kwa tofauti ya pointi nne baada ya mechi ya pili katika kundi B, ambalo linaaminika kubeba kiasi kikubwa cha wacheza wa ligi ngumu za Afrika.
Ikiwa Nigeria watashinda mechi tatu kati ya nne zilizobakia kuanzia Agosti mwakani – ambazo mbili watacheza nyumbani, watajihakikisha kumaliza nafasi ya kwanza na kushiriki michuano ya Kombe la Dunia kwa mara ya sita.
Mpira uliomgonga beki na kumrudia Moses ulimw


0 comments:
Post a Comment