umapili Novemba 6, African Lyon walikata utepe wa vipigo kwa Simba baada ya kuibuka na ushindi wa goli 1-0 kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam mchezo ambao ulikuwa wa kwanza kwa Simba kupoteza tangu kuanza kwa ligi msimu huu.
Simba imepoteza mechi mbili mfululizo ndani ya siku nne na kuziachia pointi 6.
Tanzania Prisons imeifunga Simba kwa mara ya pili mfululizo kwenye uwanja wa Sokoine. Msimu uliopita Prisons iliifunga Simba 1-0 (21/10/2015 Tanzania Prisons 1-0 Simba), kisha Novemba 9 Prisons imeifunga Simba 2-1 kwenye uwanja huohuo mechi zote zikiwa ni za mzunguko wa kwanza.
Kipa wa Simba Vincent Angban ameruhusu magoli matatu kwenye mechi mbili mfululizo baada ya kucheza mechi sita bila wavu wake kuguswa.
Tanzania Prisons wameshinda mechi yao ya kwanza baada ya kucheza mechi 4 bila kushinda. Mara ya mwisho Prisons walipata ushindi dhidi ya Stand United (19/10/2016 Tanzania Prisons 2-1 Stand United).
Simba imepoteza mechi ya kwanza nje ya Dar, mechi ya kwanza Simba ilipoteza dhidi ya African Lyon, licha ya Simba kuwa mgeni kwenye mchezo huo bado walicheza jijini Dar kwa sababu Lyon pia wanatumia uwanja wa Uhuru kama uwanja wao wa nyumbani.
Simba imeendelea kusalia na pointi zake 35 kwenye ligi kuu Tanzania bara pointi tano mbele ya watani zao wa jadi Yanga, endapo Yanga itashinda mchezo wake wa leo (Alhamisi November 10) itabakiza pointi mbili kuifikia Simba.


0 comments:
Post a Comment