Kocha msaidizi wa Simba Mayanja amesema Prisons walibahatisha kuwafunga huku Mingange akitaja madhaifu ya Simba ailiyotumia kuwafunga
Kocha mkuu wa Tanzania Prisons Meja mstaafu Abdul Mingange amesema, aligundua Simbawalikuwa na uchovu hivyo akatumia uchovu wao kupata matokeo kwenye mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.
Kupitia Azam TV Mingange amesema kikubwa kilichoipa ushindi timu yake ni kujituma kwa wachezaji na kutumia vizuri nafasi zilizopatikana ikiwa ni pamoja na udhaifu wa wapinzani wake ambapo yeye alisema ni uchovu.
Simba ni timu nzuri naiheshimu imepata nafasi ya juu, hata wao ni wapambanaji lakini nafikiri walikuwa na uchovu kwa jinsi nilivyowaona,” amesema kocha huyo aliyewahi kuhudumu kwenye klabu za Ndanda na Mbeya City kabla hajatua Prisons.
“Nawapongeza wachezaji wangu wamepigana kwa sababu sisi tunakosa matokeo lakini si kwamba timu inacheza vibaya. Leo waliniahidi watapamabana na kweli wamefanya kazi.”
“Mechi zote tunacheza vizuri lakini tulikuwa hatutumii vizuri nafasi za kufunga, leo tumefunga katika nafasi ngumu sana kwahiyo nadhani wachezaji wameamua kubadilika na kuongeza umakini.”
Kwa upande wa Simba baada ya kuchezea kichapo cha bao 2-1 kutoka kwa ‘wajelajela’ wa Mbeya, kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja amesema, walifanya kila wawezalo ili kuondoka na pointi tatu dhidi ya wapinzani wao lakini bahati haikuwa yao.



0 comments:
Post a Comment