Follow

Timu ya Wiki Ligi Kuu Bara: Azam taabani

Azam FC ikiwa taabani Ligi Kuu Bara hali ya Simba nayo si shwari baada ya kupoteza mechi dhidi ya Lyon wikiendi iliyopita, hiki ndicho kikosi bora
Mnyama Simba amepoteza mchezo kwa mara ya kwanza kwenye Ligi Kuu bara dhidi ya African Lyon hali kadhalika  Azam hali yao siyo nzuri kwao huku bingwa mtetezi Yangaakizinduka dhidi ya Tanzania Prisons
Goal inakuletea kikosi bora cha wiki Ligi Kuu Tanzania Bara
1.Beno Kakolanya
Mlinda mlango wa Yanga, Beno ndiye aliyeibuka shujaa kwenye mchezo wa Jumapili dhidi ya Prisons alifanikiwa kuzuia penati pia alikuwa bora siku hiyo kwa kuondoa michomo hatari ya washambuliaji wa Tanzania Prisons
2.Miraji Adam
Mlinzi wa kulia kutoka Africa Lyon alionesha umairi wake mkubwa wa kuwazuia mawinga hatari wa klabu ya Simba na kuwafanya kutokuwa na madhara kwenye lango lao hali kadhalika aligongesha mwamba kwenye mchezo huo kwa adhabu ndogo kipindi cha kwanza 
3.Haji Mwinyi
Mlinzi huyu amezidi kuimarika kila siku, dhidi ya Prisons alikaba na kupandisha timu kwa wakati pia aliweza kutimiza vizuri majumu yake ikiwemo kupiga krosi nyingi ambazo washambuliaji wake walishindwa kuzitumia vizuri
4.Asante Kwesi
Mlinzi huyu wa kati raia wa Ghana amekuwa na mwelekeo mzuri ndani ya kikosi cha Mbao Fc, Mghana huyu alikuwa mgumu kupitika kirahisi na washambuliaji wa Azam
5.Hassan Isihaka
Beki mahiri wa African Lyon ambaye ameendelea kuwa na msaada mkubwa kwenye kikosi cha kocha Mreno, Isihaka ndiye aliyekuwa kikwazo kwa washabuliaji wa Simba kuonekana ni butu kwani alifanikiwa kuondoa mipira yote ya hatari langoni mwao 
6.Jonas Mkude
Licha ya kupoteza mchezo na African Lyon, kiungo huyu mkabaji ndiye mchezaji pekee aliyekuwa na uhai ndani ya kikosi siku ya Jumapili kiungo huyo aliweza kufanya kwa ufasaha kazi yake na kuwapa wakati mzuri mabeki wake wa kati na kusambaza mipira vizuri kwa washambuliaji ambayo haikutumiwa sawasawa
7.Venance Ludovic
Alifunga goli moja dhidi ya Azam kwenye ushindi wa goli mbili kwa moja, kiungo mshambuliaji wa Mbao Fc amezidi kuwa chachu ya mafanikio ndani ya klabu hiyo 
8.Haruna Niyonzima
Kiungo mshambuliaji wa Yanga raia wa Rwanda alifanikiwa kulitawala eneo la kati kwa kuwazidi maarifa viungo wa Prisons alitimiza majukumu yake kwa asilimia zote uwanjani
9.Themi Felix
Mshambuliaji wa Kagera ambaye ameendelea kufanya vizuri msimu huu baada ya kuisaidia timu yake kupata ushindi wa bao 3-1 dhidi ya RUVU Shooting,Themi Felix amekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha msimu huu na huenda msimu ujao akaondoka na kujiunga na timu kubwa 
10. Donald Ngoma
Ngoma ameendelea kufanya vizuri kwa msimu huu wa Ligi Kuu baada ya kusaidia timu yake kuibuka na ushindi wa goli moja kwa bila na Tanzania Prisons alikuwa mwiba kwenye lango la maafande hao na kuwapa wakati mgumu kwao kumzuia hivyo kuishia kumchezea madhambi kila muda
11.Ahmed Msumi
Winga wa Ndanda  ambaye alitoa usumbufu mkubwa Jumapili dhidi ya Stand united aliweza kufanikiwa kufunga goli moja kwenye ushindi wa goli 2 kwa 1 dhidi ya wapiga debe wa Shinyanga 
Instagram Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment

picture of the week

picture of the week

NI LIVERPOOL DHIDI YA WTAKATIFU MANE KUKUTANA NA TIMU YAKE KWA MARA YA KWANZA

NI LIVERPOOL DHIDI YA WTAKATIFU MANE KUKUTANA NA TIMU YAKE KWA MARA YA KWANZA