Anastaili kucheza klabu kubwa kama Simba kutokana na uwezo aliouonyesha kwenye timu ndogo ya African Lyon
Klabu ya Simba ipo katika mpango wa kumsajili kipa wa African Lyon Youthe Rostand raia wa Cameroon ambaye ameonyesha uwezo mkubwa kwenye mzunguko wa kwanza wa ligi ya Vodacom Tanzania.
Kocha Joseph Omog, ameiambia Goal, yupo kwenye mazungumzo na kipa huyo kuona kama anaweza kufanikiwa kumsajili baada ya kuvutiwa na kazi yake kwenye mechi za mzunguko wa kwanza.
“Uongozi ulinipa kazi ya kutafuta kipa mwingine ambaye atasaidiana na Vicent Angban na kama kocha nimempendekeza Rostand, kwasababu hata usajili wake hataprosesi zake za usajili hazitasumbua kama ambavyo tungesajili kipa mwingine kutoka nje,”amesema Omog.
Omog amesema hajampendekeza kipa huyo kwasababu ni raia mwenzake wa Cameroon, bali ni kutokana na uwezo wake ambao amekuwa akiuonyesha kwenye ligi na hasa kwenye mchezo wao ambapo Simba ilipoteza kwa bao 1-0, uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Amesema ukitoa makosa ya timu nzima kipa huyo ameweza kufanya vizuri na kutoa mchango mkubwa kwa timu hiyo ambayo imepanda msimu huu kushiriki ligi ya Vodacom na anastaili pongezi kutokana na aina ya timu anayoichezea.
“Kwangu mimi anafaa kuichezea Simba kwasababu amekuwa na mchango mkubwa kwa Lyon, na ndiyo alikuwa kikwazo cha sisi kukosa ushindi tulipocheza nao na kutunfunga bao 1-0 pale Uwanja wa Uhuru,”amesema Omog.
Endapo Rostand atatua Simba kunauwezekano mkubwa Angban raia wa Ivory Coast akaondoka simbazi kumpisha kipa huyo mwenye umbo refu anapokuwa langoni.
Sababu kubwa inayomuondoa Angban ni kuruhusu mabao ya kizembe katika michezo miwili ya mwishoni mwa mzunguko wa kwanza ambapo timu yake ilipoteza na kubakiza pointi mbili dhidi ya mahasimu wao wa jadi Yanga ambao wanashika nafasi ya pili.


0 comments:
Post a Comment