Follow

ALABA KUJIUNGA NA MAN UNITED MAJIRA YA JOTO

Jose Mourinho bado hajapata kikosi anachokitaka United, kwa mujibu wa habari ametuma skauti kumwangalia David Alaba na Baumgartlinger
David Alaba, beki wa Bayern Munich yupo kwenye rada za Manchester United na meneja Jose Mourinho kwa mujibu wa habari.
Nyota huyo raia wa Austria, mwenye umri wa miaka 24, bado ana mkataba Allianz Arena hadi 2021, na inasemekana anafuatiliwa na maskauti wa United tangu kipindi cha mapumziko ya kimataifa.
Inadaiwa na The Mirror kuwa Mourinho anatafuta beki matata wa kushoto na kiungo mkabaji – nafasi ambazo nyota huyo mahiri wa Bayern anazimudu.
Pamoja na kumfukuzia Alaba, habari hizo hizo zimedai kuwa mchezaji mwenzake wa Austria Julian Baumgartlinger pia yumo kwenye rada za Mashetani Wekundu -  hii inamaanisha siku za Morgan Schneiderlin zinahesabika Old Trafford.
Alaba pia yupo kwenye rada za Real Madrid, wakati Baumgartlinger – ambaye ndio kwanza amjiunga na Bayer Leverkusen akitokea Mainz 05 majira ya joto – anakodolewa macho na klabu tele za barani Ulaya.
Jose Mourinho alianza kibarua chake Manchester United kwa kushinda mechi tatu mfululizo, lakini ameshinda mechi mbili tu kati ya tisa zilizofuata na walibanwa kwa sare ya tatu mfululizo nyumbani baada ya kutoa sare dhidi ya Arsenal Jumamosi.
Bao la Olivier Giroud la dakika ya 89 ambalo aliliweka kimiani kwa kichwa ilikuwa jitihada pekee waliyofanya Arsenal kusawazisha goli lililowekwa kambani na Juan Mata ambalo liliwapa Manchester United uongozi katika mechi hiyo.
Licha ya yote, Carrick ambaye alikuwa nahodha wa Mashetani Wekundu wakati Wayne Roone akianzia benchi, anaamini kwamba klabu hiyo itarejea kwenye mbio za ushindi muda si mrefu.
“Kila mchezo ambao unaamini unahitaji kuwa na kiwango kikubwa – ni sharti iwe hivyo, ni vema kupambana zaidi kupata matokeo,” kiungo huyo alikiambia MUTV. “Si jambo rahisi kukubaliana na matokeo kama yale wakati unapokuwa umecheza vizuri, umefanya kila jambo na unastahili kupata ushindi.
“Nadhani tatizo linakuja pale unapokuwa umepanga mambo na hayaendi kama unavyotaka, na unadhani ungefanya vema zaidi, tulipaswa kuwa katika ubora wetu zaidi na kuna matatizo machache tunahitaji kuyatatua.
“Kwa kweli sioni matatizo tunayolazimika kutatua. Sidhani kama matokeo ndilo tatizo kubwa, lakini tukicheza vile mara zote, nadhani tunaweza kushinda mechi nyingine nyingi zaidi tusipopoteza nafasi. Naamini hilo linakwenda kutokea sasa na hadi mwisho wa msimu.”
United wanashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu Uingereza kufuatia sare ya 1-1 dhidi ya Arsenal katika dimba la Old Trafford.
Instagram Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment

picture of the week

picture of the week

NI LIVERPOOL DHIDI YA WTAKATIFU MANE KUKUTANA NA TIMU YAKE KWA MARA YA KWANZA

NI LIVERPOOL DHIDI YA WTAKATIFU MANE KUKUTANA NA TIMU YAKE KWA MARA YA KWANZA