Follow

Nasri: "Guardiola huzuia wachezaji kufanya ngono usiku"

Pep Guardiola amekuwa kocha wa kipekee mwenye masharti na kanuni kali ili kuwawezesha wachezaji wake kufanya vizuri dimbani
Samir Nasri amefunguka kuwa Pep Guardiola, meneja wa Manchester City amewakataza wachezaji wake kufanya mapenzi usiku wa manane ili kuepuka kujeruhi misuli.
Kocha huyo raia wa Hispania anafahamika kwa masharti makali, ambayo ni pamoja na kuizuia timu kutumia vyakula vya anasa na kuwatoa kwenye mazoezi ya kikosi cha kwanza ikiwa hawafuati maelekezo yake.
Nasri alikuwa moja ya wachezaji ambao Guardiola alisema wamezidi uzito, na kumtoa kwa mkopo kwenda Sevilla majira ya joto.
Katika mahojiano na L'Equipe du Soir, Nasri alizungumzia utendaji wa meneja huyo akidai kuwa nyota wa Barcelona Lionel Messi na Robert Lewandowski mshambuliaji wa Bayern Munich walifanikiwa kung’ara chini ya kocha huyo kwa sababu walizuiwa kufanya mapenzi.
“Mapenzi ni lazima yafanyike kabla ya usiku wa manane. Hata kama una nafasi ya mapumziko siku inayofuata,” alisema Nasri.
“Alituambia hivyo ndivyo alivyofanikiwa kupata matokeo mazuri kutoka kwa Messi na Lewandowski, ni ili waepuke majeraha ya misuli. Kwa kufanya hivyo unapata muda wa kutosha kulala usiku.”
Arsene Wenger meneja wa Arsenal, amebainisha kuwa uwanja wake pendwa wa mpira wa miguu ni ule unaomilikiwa na wapinzani wake wa ligi, Liverpool.
Mfaransa huyo ambaye amekuwa akiinoa Gunners kwa muda wa miaka 20 sasa, amesifia hali inayorindima kwenye uwanja wa Anfield katika mechi za Liverpool.
Klabu hiyo ya Merseyside imeongeza uwezo wa uwanja huo hadi kufikia idadi ya watu 54,000 kwa kuuboresha zaidi majira ya joto.
“Uwanja wangu pendwa na wenye mashabiki na uliochangamka sana ni Liverpool kwa sababu kuna upepo wa kipekee hapa,” Wenger alikiambia beIN Sports. “Wimbo kabla ya mechi, ‘You will Never Walk Alone’, historia ya klabu na uwanja kadhalika.
“Kabla ya hapo ilikuwa Highbury, kulikuwa na hali ya kipekee. Sasa ni Everton, Liverpool, Newcastle ambayo pia ilikuwa safi. Soka ni sawa na ilivyokuwa miaka 30 iliyopita kwa sababu a mazingira ya mchezo waenyewe. Huba, mwamko viwanjani. Anfield pamechangamka sana, na hali ya ushirikiano.
Wenger atazuru Anfield akiwa na timu yake Machi 4 timu hizo zitakapokwaana kwenye Ligi Kuu Uingereza.
Instagram Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment

picture of the week

picture of the week

NI LIVERPOOL DHIDI YA WTAKATIFU MANE KUKUTANA NA TIMU YAKE KWA MARA YA KWANZA

NI LIVERPOOL DHIDI YA WTAKATIFU MANE KUKUTANA NA TIMU YAKE KWA MARA YA KWANZA