Follow

Cruyff: "Depay anahitaji dakika zaidi Manchester United"

Cruyff anaamini Memphis Depay bado hajaisha, anaweza kufanya vizuri zaidi Manchester United kama atapewa nafasi zaidi
Kiungo wa zamani wa Manchester United Jordi Cruyff amesema kuwa winga anayehahaMemphis Depay anahitaji kupewa muda zaidi wa kucheza.
Depay aliwasili Manchester United mwaka jana baada ya muda mrefu kuzungumziwa kama mchezaji bora duniani kwa siku zijazo, lakini ameshindwa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza United licha ya klabu kuendelea chini ya utawala wa makocha wawili katika kipindi chake kwenye Ligi Kuu Uingereza.
Cruyff, ambaye alidumu misimu minne Old Trafford, haamini kama amali ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ndio imeishia hapo United, lakini, badala yake amesema Jose Mourinho anahitaji kumpa mchezaji huyo kinda fursa ya dakika zaidi kucheza dimbani ili kumsaidia kuendeleza kipaji chake.
“Kwa hakika, United ni klabu kubwa na yenye mafanikio, lakini nadhani pia Depay ni mchezaji mahiri,” Cruyff alikiambia Gulf News.
“Kitakwimu, hapati muda wa kutosha dimbani, lakini sijui muda anaoingia mchezoni na kutoka. Lakini kwa hakika, ana uwezo mkubwa na ameonesha hilo.
“Sasa mbinu ni kuhakikisha anapata fursa ya kucheza japo kila wiki. Hatimaye atakuwa bora zaidi, lakini haijulikani ni wapi na lini.”
Depay amecheza mechi 33 Manchester United, akifunga mabao mawili katika mechi hizo
Instagram Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment

picture of the week

picture of the week

NI LIVERPOOL DHIDI YA WTAKATIFU MANE KUKUTANA NA TIMU YAKE KWA MARA YA KWANZA

NI LIVERPOOL DHIDI YA WTAKATIFU MANE KUKUTANA NA TIMU YAKE KWA MARA YA KWANZA