Henrikh Mkhitaryan ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa nchi yake kama thawabu ya kiwango kikubwa alichoonyesha kwa nchi na klabu zake
Kiungo wa Manchester United Henrikh Mkhitaryan amekiri kuwa amepania kuweka historia katika klabu hiyo baada ya kujihakikishia nafasi kwenye kikosi cha timu hiyo.
Nyota huyo raia wa Armenia katika umri wa miaka 27, amekuwa mchezaji bora wa mwaka wa taifa lake kwa mara ya sita mfululizo Jumatano mchana, kufuatia kiwango chake safi cha 2015/16 akiwa Borussia Dortmund kabla ya kutua Old Trafford majira ya joto.
Mkhitaryan, ambaye tayari ameshashinda tuzo binafsi mara saba, anatumaini kuendelea kutisha Manchester United miezi ijayo na miaka ili aweze kukuza jina lake katika klabu hiyo chini ya uongozi wa meneja Jose Mourinho.


0 comments:
Post a Comment