Mbwana Samatta ameibuka upya baada ya kutupia mbili kuiwezesha timu yake kupata ushindi muhimu wa 3-1 dhidi ya Waasland-Beveren
Karelis amekuwa akimpa wakati mgumu Mbwana Samatta pale Genk kwani yeye ndiye mshambuliaji tishio zaidi na mwenye uwezo wa kubadili matokeo muda wowote kwa klabu hiyo ya Ubelgiji.
Lakini Mbwana Samatta amejikomboa wiki hii baada ya kufanikiwa kupiga bao mbili wakati KRC Genk ikipata ushindi wa ugenini wa magoli 3-1 dhidi ya Waasland-Beveren katika mchezo wa kuwania taji la Croky.
Mchezaji wa kimataifa wa Tanzania, Samatta alianza kufunga goli la kwanza dakika ya 15 kabla ya kurejea tena kambani dakika tatu kabla ya kwenda mapumziko huku bao la tatu la Genk likipachikwa wavuni na Wilfred Ndindi dakika ya 80.
Bao pekee la Waasland-Beveren likifungwa dakika ya 89 kupitia kwa Zinho Gano.
Imeripotiwa kuwa kiungo wa Arsenal Santi Cazorla ameshauriwa na madaktari kufanyiwa upasuaji wa mguu kutatua tatizo linalomkabili.
Muhispania huyo hajapata nafasi ya kutia mguu dimbani tangu alipopata majeraha Arsenal iliposhinda 6-0 dhidi ya Ludogorets Razgrad Oktoba 19.
Tatizo hapo awali halikuonekana kuwa bay asana, lakini kadiri muda unavyoenda inaonekana uponaji wake umekuwa duni, na kwa mujibu wa IBTimes UK, Madaktari bingwa wa Ulaya wamemshauri Cazorla kuwa tiba ya upasuaji ndilo jibu pekee kwa tatizo lake.
Cazorla mwenye umri wa miaka 31 iwapo atapigwa kisu, haitawezekana kurejea kwenye kikosi cha Arsenal hivi karibuni timu hiyo inapokabiliwa na majukumu mazito ya msimu wa Krismasi na Mwaka Mpya.
Imefahamika kuwa Arsenal watafanya maamuzi siku chache zijazo kama wamfanyie tiba hiyo ya upasuaji au la!


0 comments:
Post a Comment