Follow

MO Ibrahim amemshawishi Mkwasa kumpanga kikosi cha Stars

Charles Mkwasa amemwaita kwa mara ya kwanza Mohamed Ibrahim na wachezaji wengine watatu waliofanya vizuri Ligi Kuu hadi sasa
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ ameita kikosi cha wachezaji 24, kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Zimbabwe utakaopigwa Harare Novemba 13, 2016.
Mchezo huo upo katika utaratibu wa kalenda ya Shirikisho la soka duniani FIFA ambapo inachangia kupanda kwa viwango vya nchi endapo inafanya vizuri hasa katika mechi za kimataifa.
Mkwasa ameiambia Goal, anaimani kubwa na wachezaji hao baada ya kuwafuatilia kwa makini kwa kipindi chote ambacho ligi ya Vodacom Tanzania imekuwa ikichezwa .
Mkwasa amesema kikosi hicho kitaingia kambini Novemba 7 na watafanya mazoezi kwa muda wa siku kadhaa kabla ya kusafiri kwenye Harare kwa ajili ya pambano hilo ambalo amekusudia kushinda.
“Tumewachagua Zimbabwe kwa sababu ni timu iliyo juu yetu kwenye viwango vya FIFA, na hawa wanashiriki fainali za AFCON mwaka huu na tunaamini mchezo utakuwa mgumu na tunaweza kupata matokeo,” amesema Mkwasa.
Katika uteuzo huo wa wachezaji Mkwasa amewajumuisha kwa mara ya kwanza wachezaji Mohamed Ibrahim 'Mo' wa Simba, James Josephat wa Tanzania Prisons, Abrahaman Musa na Omar Mponda kutokana na kuonyesha kiwango cha juu kwa timu zao.
Wachezaji walioitwa na Mkwasa kuunda kikosi cha Stars ni:
 Makipa: Said Kipao, Deo Munishi na Aishi Manula.
Mabeki: Michael Aidan, Erasto Nyoni, Mohamed Husein, Haji Mwinyi, Andrew Vicent, David Mwantika na James Josephat.
Viungo: Himid Mao, Jonas Mkude, Mohamed Ibrahim, Muzamiri Yassin, Simon Msuva, Shiza Kichuya, Jamal Mnyate na Abrahaman Musa.
Washambuliaji: Omar Mponda, Mbwana Samatta, John Bocco, Thomas Ulimwengu, Elias Maguli na Ibrahim Ajib.
Mwezi uliopita Tanzania haikupata mchezo wa kirafiki baada ya Ethiopia waliyopanga kucheza nayo kuahirisha dakika za mwisho kutokana na sababu za kiusalama
Instagram Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment

picture of the week

picture of the week

NI LIVERPOOL DHIDI YA WTAKATIFU MANE KUKUTANA NA TIMU YAKE KWA MARA YA KWANZA

NI LIVERPOOL DHIDI YA WTAKATIFU MANE KUKUTANA NA TIMU YAKE KWA MARA YA KWANZA