Meneja wa Arsenal Arsene Wengeramethibitisha kwamba Hector Bellerin anatarajiwa kuwa nje kwa wiki nne baada ya kupata majeraha katika mchezo dhidi ya Tottenham.
Beki huyo wa kulia Mhispania aliumia kifundo cha mguu wakati wa mchezo dhidi ya Spurs uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 kabla ya kupisha mapumziko ya mechi za kimataifa.
Katika mkutano na wanahabari leo Wenger amesema: “Hector atakuwa nje kwa wiki nne. Alipata majeraha sekunde kumi tu kabla ya mchezo dhidi ya Spurs kumalizika.”
Kwa hali hiyo Bellerin ataukosa mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Manchester Unitedunaotarajiwa kufanyika Jumapili ya wikiendi hii katika Uwanja wa Old Trafford.


0 comments:
Post a Comment