Follow

Walcott, Ozil waing’arisha Arsenal na kuikuta Man City kileleni

Theo Walcott amefunga mabao mawili kati ya matatu na kuipa timu yake ya Arsenal iliyokuwa pungufu mbele ya Swansea chini ya meneja wao mpya Bob Bradley, mchezo uliofanyika Emirates jioni ya leo.
Mshambulizi huyo wa Arsenal na timu ya taifa ya England kwa sasa ametimiza magoli matano kwenye michezo nane baada ya kufunga magoli mawili leo kwa ustadi mkubwa kufuatia makosa ya Jordi Amat na Jack Cork.
Swansea walifanikiwa kupata bao kupitia kwa Gylfi Sigurdsson baada ya kiungo wa Arsenal Granit Xhaka kufanya makosa.
Mesut Ozil aliifungia Arsenal bao la tatu baada ya kupata krosi mujarab kutoka kwa Alexis Sanchez, lakini Swansea waliapata goli la pili kupitia kwa Borja Baston aliyeingia kutoka benchi baada ya kupata pasi safi kutoka kwa Modou Barrow ambaye alikuwa mwiba mchungu kwa Arsenal leo.
Granit Xhaka alitolewa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumchezea faulo mbaya Modou Barrow.
Instagram Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment

picture of the week

picture of the week

NI LIVERPOOL DHIDI YA WTAKATIFU MANE KUKUTANA NA TIMU YAKE KWA MARA YA KWANZA

NI LIVERPOOL DHIDI YA WTAKATIFU MANE KUKUTANA NA TIMU YAKE KWA MARA YA KWANZA