Follow

CHELSEA YAMTANGAZA Batshuayi RASMI

helsea imetangaza usajili wa mshambuliaji wa Ubelgiji Michy Batshuayi kutoka Marseille
Nyota huyo wa miaka 22 amekuwa akifukuziwa na Tottenham na Crystal Palace, amesaini mkataba wa miaka miano na Blues baada ya kurejea kutoka Euro 2016 alipokuwa akiiwakilisha nchi yake.
Inaaminika kwamba mshambuliaji huyo ameigharimu Chelsea takribani paundi milioni 33.2.
“Nafurahi kufanya mkataba na moja ya klabu kubwa katika Ulaya na ninafungua ukurasa mpya wa maisha yangu. Natumai naweza kuisaidia Chelsea kushinda mataji mengi muda wote nitakaokuwa Darajani Stamford,” aliiambia tovuti rasmi ya klabu.
“Eden Hazard na Thibaut Courtois wameniambia mambo mengi kuhusu klabu hii, na ukijumlisha na ujio wa Antonio Conte, nadhani ni wakati mwafaka kwangu kuwa mchezaji wa Chelsea. Hii ni fursa ya kipekee sana kwangu na familia yangu, nasubiri kwa hamu kucheza Ligi Kuu Uingereza msimu ujao.”
Instagram Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment

picture of the week

picture of the week

NI LIVERPOOL DHIDI YA WTAKATIFU MANE KUKUTANA NA TIMU YAKE KWA MARA YA KWANZA

NI LIVERPOOL DHIDI YA WTAKATIFU MANE KUKUTANA NA TIMU YAKE KWA MARA YA KWANZA