Follow

Ndayragije: Mechi ya Mbao dhidi ya Azam ni kama fainali

Mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu na wenye ushindani wa aina yake kwani Mbao hawajapata ushindi kwenye mechi nne walizocheza hivi karibuni
Baada ya kushinda mechi mbili za ugenini kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa kocha wa Azam FC, Zeben Hernandez hamasa waliyokuwa nayo hivi sasa itawasaidia kushinda mchezo wao wa kesho dhidi ya Mbao FC.
Pambano hilo limepangwa kupigwa uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza huo ukiwa ni mchezo wa tatu mfululizo baada ya kuzifunga Kagera Sugar, Toto African  na kesho ni zamu ya Mbao.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu na wenye ushindani wa aina yake kwani Mbao hawajapata ushindi kwenye mechi nne walizocheza hivi karibuni na mbaya zaidi wataingia kwenye mchezo huo wakitoka kufungwa mabao 2-0 na Kagera Sugar Jumatano iliyopita.
Kocha Ettiene Ndayiragije, amesema mchezo huo ni kama fainali kwao kuhakikisha wanarudisha mwendelezo wa kupata matokeo mazuri kama ilivyokuwa kwenye mechi walizocheza siku za nyuma
“Nafahamu Azam ni timu kubwa na nzuri lakini tumejipanga kufanya tunashinda mchezo huo ukizingatia tunacheza nyumbani mbele ya mshabiki wetu na kitu kingine kizuri tunataka kuwaonyesha mashabiki wetu kwamba kupoteza mechi zilizopita kulitokana na uchovu na siyo kuzidiwa,”amesema Ndaliyagije.
Instagram Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment

picture of the week

picture of the week

NI LIVERPOOL DHIDI YA WTAKATIFU MANE KUKUTANA NA TIMU YAKE KWA MARA YA KWANZA

NI LIVERPOOL DHIDI YA WTAKATIFU MANE KUKUTANA NA TIMU YAKE KWA MARA YA KWANZA